Oman washerehekea siku ya Taifa hilo

0
90

Taifa la Oman, leo linasherehekea miaka 52 tangu kuasisiwa kwake.

Mbali na kusherehekea miaka hiyo 52 tangu kuasisiwa kwake, wananchi wa Oman pia wanasherehekea mafanikio makubwa yaliyofikiwa chini ya uongozi wa Sultani Haitham Bin Tariq.

Raia wa Oman wanamtaja Sultani Haitham Bin Tariq kuwa ni kiongozi ambaye amekuwa akifanya juhudi kubwa katika kuiimarisha Oman kisasa, kimaendeleo na kiuchumi, na kumfanya kila mwananchi wa Taifa hilo awe
mshiriki wa kweli wa maendeleo jumuishi.

Taarifa iliyotolewa na Oman kwa vyombo vya habari katika kusherehekea miaka 52 ya Taifa hilo imetaja mageuzi mbalimbali yanayofanywa, ili kuhakikisha Taifa hilo linasonga mbele.

Mageuzi hayo ni pamoja na yale yanayoendelea kuelekea kwenye mfumo wa kidijatali wa Serikali, ikiwa ni moja ya programu za utekelezaji wa uchumi wa kidijiti ambayo ni nyenzo kuu za kusaidia kufikia vipaumbele vya dira ya Oman ya mwaka 2040.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mtazamo wa
Sultani Haitham Bin Tariq umejikita katika kuendeleza azma ya Oman ya kuwa na ushirikiano chanya na watu wote katika nyanja zenye manufaa na ambazo zitakuza masilahi ya pande zote.

Matokeo ya mtazamo huo yamejitokeza katika ziara za viongozi mbalimbali duniani akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi.