YANGA YAZINDUA JEZI MPYA KWA KISHINDO DAR

0
486

Klabu ya soka ya Yanga ya Jijini Dar ea salaam kwa kushirikiana na kampuni ya GSM, leo wametambulisha jezi rasmi za timu hiyo watakazozitumia msimu wa 2019/20.


Hafla hiyo ya utamburisho wa jezi hizo mpya imefanyika leo asubuhi kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa Yanga Dr Mshindo Msolla amesema kuwa hizo ndiyo jezi rasmi na halali za Yanga watakazozitumia katika msimu ujao.

Msolla amesema kuwa, jezi hizo zina ubora mkubwa kulinganisha na jezi nyingine zilizowahi kuvaliwa na wachezaji wa klabu hiyo miaka ya nyuma.

“Hakuna jezi yenye ubora kama huu nchini Tanzania. Pia tutafungua duka kubwa la vifaa mbalimbali vyenye nembo ya Yanga, hamjawahi kuona duka la Kimataifa kama hilo,” amesema Msolla.

Mkurugenzi wa GSM, Hersi Said amesema “Hakuna jezi yenye ubora kama huu tuliouzindua leo hapa nchini, baada ya uzinduzi huo tutafungua duka kubwa la vifaa mbalimbali vyenye nembo ya Yanga ambalo halijawahi kutokea hapa nchini.