Wanawake watatu mbaroni kwa kuwalewesha na kuwaibia wanaume baa

0
196

Polisi huko Nyeri, nchini Kenya wanawashikilia wanawake watatu wanaodaiwa kuibia wanaume katika kumbi za starehe.

Wanawake hao wanaojulikana kwa majina Rita Okuto, Caroline Kariuki na Caroline Wanjiku walikamatwa usiku wakiwa wanazunguka nje ya muda watu wanaoruhusiwa kuwa nje baada ya Kenya kuweka “Lockdown”.

Watuhumiwa walikutwa na simu sita, tablet, tarakilishi mpakato (laptop) pamoja na vitambulisho, kadi za ATM za watu wengine pamoja na dawa zinazosadikiwa kutumika katika kuwafanya wahanga wao kusinzia kabla ya kuwaibia.

Wanaume wawili walijitokeza kushitaki katika kituo cha polisi Njeri na kufanikiwa kupata simu zao na kusema kuwa walikuwa na wanawake hao baa.

Washitakiwa watafikishwa mahakamani Aprili 6, kwa ajili ya kusomewa mashitaka.