Wanasa katika tope na kufariki dunia

0
294

Watu wanne wa familia moja wakazi wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, wamefariki dunia baada ya kuzama katika dimbwi lililopo kwenye mto Mzinga.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Pwani, -Wankyo Nyigesa amesema  watu hao wakazi wa kitongoji cha Amani walizama na kunasa katika tope wakati wakivua samaki kwenye dimbwi hilo.

Amesema watu hao walifariki dunia wakati wakijaribu kumuokoa mwenzao ambaye awali alitumbukia katika dimbwi hilo, na walipoingia kwa bahati mbaya ndipo nao wakanasa katika tope na kushindwa kujiokoa.

Amewataja waliofariki dunia katika tukio hilo kuwa ni Jumla Matonange, Emanuel Matonange, Ashura Emanuel na Felister Charles.