Wakorea kurudisha umri nyuma

0
111

Wakati watu wakizeeka kadri miaka inavyoongezeka, Wakorea Kusini wanakadiriwa kuzidi kurudi utotoni kwa mwaka mmoja au miwili.

Hiyo ni kwa sababu bunge la nchi hiyo limepitisha sheria mpya ya kuondoa mifumo yao mitatu ya kuhesabu umri na kufanya iende sawa na mfumo wa namna dunia inahesabu umri.

Mifumo hiyo mitatu ya ni; umri wa kimataifa, umri wa Korea na umri wa kalenda.

Hiyo ina maana kwamba Wakorea Kusini wana umri mitatu tofauti, kulingana na nani anayeuliza. Kuanzia Juni 2023, watatumia rasmi umri wao wa kimataifa pekee, ambao unahesabu kutoka 0 tarehe ya kuzaliwa.

Kwa sasa, Wakorea Kusini wengi hutumia “umri wao wa Kikorea” katika mazingira mengi yasiyo rasmi. Chini ya njia hii, Wakorea wana umri wa mwaka mmoja wakati wanazaliwa. Mwaka mwingine huongezwa kwa umri wa mtu kila Januari 1, kwa hiyo, kwa mfano, mtoto aliyezaliwa mnamo Desemba 31 atakuwa na umri wa miaka miwili siku inayofuata.