Utafiti mpya wa mbolea waonesha mafanikio

0
180

Mtafiti wa Masuala ya Ikolojia Profesa Stephen Ketaro amesema mafanikio yameanza kupatikana katika utafiti wa uzalishaji na uchakataji wa mbolea asilia (NPK).

Mbolea hiyo ambayo huzalishwa kwa kutumia malighafi asilia imefanyiwa utafiti na Profesa Katero na majaribio yake yameonesha kuwa na mafanikio kwa wakulima ambao wameanza kuitumia kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza mkoani Dar es salaam, wakati wa ziara ya mafunzo ya Mbunge wa Mufindi Kusini David Kihenzile, Profesa Katero amesema, majaribio ya mbolea hiyo yamezaa matunda kwani imeweza kuboresha aina mbalimbali za udongo na kuwawezesha wakulima kupata mazao bora.

Kwa upande wake Mbunge Kihenzile ameomba teknolojia inayotumika kuzalisha mbolea hiyo kupelekwa kwa wakulima wa Mufindi ili kuwawezesha kuitumia na kupata tija katika mazao yao.