Ushirika si chimbo la kujipatia fedha

0
174

Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda, amewataka viongozi kuacha kuutazama Ushirika kama machimbo ya kutafuta fedha badala yake wawe chachu ya kuhakikisha Ushirika unakua kwani Ushirika ni mali ya wanaushirika.
 
Profesa Mkenda ameyasema hayo mjini Moshi, wakati akifungua Kongamano la pili la kimataifa kwa Maendeleo ya ushirika, na kuongeza kuwa serikali inataka kuziba mianya hiyo sambamba na kuwachukulia hatua viongozi katika vyama ambavyo havifanyi vizuri.
 
Amesema kazi ya Viongozi wa Ushirika ni kujijengea mazingira ili wanaotaka kujiunga na ushirika wajiunge na wamiliki ushirika wao na wauendeshe kwa matakwa yao bila kuvunja sheria wala kuingiliwa ingiliwa.
 
Mrajisi wa vyama vya ushirika nchini, Dokta Benson Ndiege, amesema kwa sasa wanahamasisha vyama vya ushirika, viweze kuanzisha viwanda ambavyo vitaongeza thamani ya mazao wanayozalisha ili kujiletea maendeleo
 
Baadhi ya washiriki katika kongamano hili wamesema iwapo wanaushirika watawezeshwa kuzalisha malighafi, kuchakata pamoja na kuuza bidhaa iliyokamilika itasaidia kufikia uchumi wa kati wa juu.
 
Kongamano hili linawashirikisha Wadau, wataalamu na watafiti mbalimbali wa Ushirika kutoka ndani na nje ya nchi lenye maudhui ya Ushirika kwa maendeleo ya viwanda na kumuweka mwanaushirika katikati