Ujenzi wa uwanja Arusha wafikia 16%

0
99

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa michezo wa Arusha unaotarajiwa kutumika kwa katika Fainali za AFCON 2027 unaendelea vizuri ambapo umefikia asilimia 16 za ujenzi.

Msigwa amesema hayo leo Desemba 21, 2024 wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi huo unaojengwa Olmoti mkoani Arusha.

Msigwa amesema mradi huo utagharimu shilingi Bilioni 286 hadi kukamilika kwake na Rais Samia Suluhu Hassan ameshatoa maelekezo na fedha zinatoka kwa wakati.

Katika hatua nyingine, Msigwa amesema hivi karibuni atatoa taarifa rasmi kuhusu ujenzi wa uwanja wa michezo wa Dodoma.