TCRA yatoa mwongozo wa maudhui ya maombolezo

0
199

Kufuatia kifo cha Rais, Dkt. John Magufuli, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevitaka vituo vyote vya utangazaji vinavyorusha maudhui ya ndani na vyenye leseni iliyotolewa na mamlaka hiyo kurusha maudhui ya maombolezo katika kipindi chote cha maombolezo.

Aidha, kwa mujibu wa Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Maudhui ya Utangazaji na Redio na Televisheni) 2018 vituo vyenye leseni za kijamii na kiwilaya vimetakiwa kujiunga (hook) na chombo cha umma cha utangazaji (TBC1 na TBC Taifa) au kituo chochote chenye leseni ya kitaifa ili kuendelea kuwahabarisha wananchi matukio muhimu ya maombolezo.