TBC na Sauti ya Nigeria zasaini hati ya makubaliano

0
354

Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Sauti ya Nigeria (VON) wamesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano katika maeneo matano ambayo ni kubadilishana ujuzi, kukuza lugha ya Kiswahili, kubadilishana wafanyakazi, kubadilishana maudhui na kupata wawakilishi wa vyombo vya habari husika yani TBC na VON.

Makubaliano hayo yamesainiwa leo Julai 12, 20024 na Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt. Ayub Rioba na Mkurugenzi Mkuu wa VON, Jibrin Baba Ndace katika ofisi za TBC Mikocheni mkoani Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kusainiwa kwa hati hiyo ya makubaliano Dkt. Rioba amesema makubaliano hayo yatasaidia kukuza ajenda za Kiafrika kutokana na umuhimu ulioonekana kwa waafrika wenyewe kuelezea masuala yanayowahusu kwa mtazamao wa Afrika.

Kwa upande wake Ndace amesema makubaliano hayo ni muendelezo wa ushirikiano baina ya Tanzania na Nigeria ambao umedumu kwa muda mrefu.