Rwanda imetangaza Kuwa mpaka wake mkubwa na Uganda ambao ulikuwa umefungwa toka mwaka 2019 utafunguliwa tena kuanzia Jumatatu.
Watu kuvuka mpakani na kusafirisha biashara katika mpaka wa Gatuna na Katuna kulisimamishwa kutokana na mvutano kati ya nchi hizo mbili.
Bidhaa tu ziliruhusiwa kupitia mipaka mingine miwili midogo ya Cyanika na Kagitumba.
Kufunguliwa upya kwa mpaka huo kulitangazwa baada ya mtoto wa Rais Yoweri Museveni Luteni Generali Muhoozi Kainerugaba kukutana na Rais Paul Kagame nchini Rwanda mwishoni mwa juma.
Rwanda iliishutumu Uganda kuwakamata na kuwarudisha raia wake na kuwaunga mkono waasi kutoka vikosi vya DFLR.
Serikali ya Uganda imekana shutuma hizo na kuishutumu Rwanda kuingilia vikosi vyake vya ulinzi.