Rais Magufuli ateua makatibu wakuu wa wizara ya mbili

0
452
Balozi (Kanali) Wilbert Augustine Ibuge

Rais John Pombe Magufuli amemteua Balozi (Kanali) Wilbert Augustine Ibuge kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Kabla ya uteuzi huo Balozi Ibuge alikuwa Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocal) katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Uteuzi wa Balozi Ibuge unaanza leo tarehe 06 Februari, 2020.

Balozi Ibuge anachukua nafasi ya Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe ambaye amehamishwa wizara kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Dkt. Mnyepe anachukua nafasi ya Dkt. Frolence Turuka ambaye amestaafu. Uteuzi wa Mkuu wa Itifaki utafanywa baadaye na tarehe ya kuapishwa kwa Balozi Ibuge itatangazwa baadaye.