Rais Samia Suluhu Hassan amesema, nchi lazima ikope ili kuendeleza miradi mikubwa ya maendeleo na tayari mifuko na wafadhili kadhaa wamekubali kuipa nchi Zaidi ya shilingi Trilioni 7 kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo.
Akihutubi wakati wa hafla ya kupokea taarifa ya Matumizi ya Fedha za Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO -19, Rais Samia Suluhu Hassan amesema Mikopo ni lazima na tozo zitaendelea ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Rais amesema, jambo linaloisukuma serikali yake kukopa ni kuendeleza maendeleo ya watu na Tanzania itakopa mikopo yenye riba nafuu na itakuwa makini na mikopo inayochukua.
Kuhusiana na madeni ya nchi Rais amesema, serikali italipa madeni yaliyoiva ili kuendelea kulipa kutoa fursa kwa Tanzania kulipa madeni mengine na kutoa huduma kwa watanzania.
Kuhusiana na wanaolalamika juu ya serikali yake kukopa Rais amesema, hataacha kukopa kwa maendeleo ya watanzania n ahata kuwa Rais wa kwanza kukopa kwa ajili ya watanzania.
Ameshangazwa pia na viongozi wanalalamikia mikopo na kuwashabiisha viongozi hao na tamaa ya urais hivyo wanatafuta maneo ya kukatisha tamaa na kufifiisha jitihada zake za kuwaletea wananchi maendeleo.
Aidha Rais amesema hivi karibuni atatoa orodha mpya ya viongozi ambao yeye anaona wanastahili kumsaidia kazi na kwamba wale ambao wanajipanga kwa urais wa 2025 hawatakuwa na nafasi katika serikali yake.