Jeshi la Polisi nchini Kenya linawashilikia watu Sita baada ya kukamata zaidi ya Dola Milioni 20 za Kimarekani ambazo ni bandia katika tawi moja la benki ya Barclays lililopo jijini Nairobi.
Katika taarifa yake, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Kenya amesema kuwa Dola hizo za Kimarekani ambazo ni bandia zilikua katika noti za Dola Mia Moja zimekutwa katika makasha ya kuhidhi fedha ya benki hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo,kati ya watu hao Sita wanaoshikiliwa na Jeshi la polisi nchini Kenya, ni mtu anayetuhumiwa kuwa ni mmiliki wa kasha lililokua na fedha hizo anayedaiwa kuwa mwekezaji na wafanyakazi wawili wa tawi hilo la benki ya Barclays jijini Nairobi.