MUHAS na uboreshaji wa kitengo cha saratani kwa watoto

0
253

Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kwa kushirikiana na Shirkiana na Shirika la Tumaini la Maisha (Global Hope) kimezindua programu itakayosaidia kuboresha utoaji huduma za afya kitengo cha saratani kwa watoto.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya uzinduzi wa programu hiyo Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Andrea Pembe amesema kuzinduliwa kwa programu hiyo ni msaada mkubwa katika kuwajengea uwezo wataalamu kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakumba watoto wenye saratani ya damu.

Kwa upande wao Mkurugenzi wa Huduma na Tiba kutoka Wizara ya Afya, Dkt.Omary Ubuguyu amesema program hiyo pia itasaidia katika kuboresha miundombunu ya utoaji huduma za Afya kitengo cha Saratani kwa watoto na maeneo mengine.

Naye mwakilishi wa Global Hope, Dkt. Aifello Wedson ameahidi kuendelea kusaidia hospitali hiyo kukabiliana na changamoto ya saratani kwa watoto kama walivyofanya kwenye nchi zingine za bara la Afrika ikiwemo Uganda.