Miradi ya maji Tanga sasa kujiendesha

0
214

Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji, Nicodemas Mkama amesema hati fungani inayozinduliwa leo inakwenda kusaidia miradi ya maji Tanga kujiendesha yenyewe.

Amebainisha hayo katika hafla ya Uzinduzi wa Hati Fungani ya Kijani ya Miundombinu ya Maji Tanga baada ya Malamka ya Maji na Usafi wa Mazingira Tanga kukidhi matakwa ya kisheria na kanuni ya uuzaji wa hati fungani kwenye masoko ya mitaji na kwa umma.

Ameongeza kuwa Mamlaka ya Masoko na Mitaji itaendelea kusimamia ipasavyo hati fungani hiyo ili kuleta mafanikio makubwa na kufungua milango kwa hati fungani nyingine katika kuchagiza maendeleo ya taifa.