Miili zaidi ya waliokufa kwa njaa yafukuliwa

0
171

Polisi nchini Kenya mpaka sasa wamefukua miili ya watu 58 waliozikwa kwenye makaburi yaliyogundulika katika eneo linalomilikiwa na Mchungaji Paul Makenzi.

Mchungaji huyo wa Kanisa la
Good News International
ambaye kwa sasa anashikiliwa na Polisi nchini Kenya, anadaiwa kuwaagiza waumini wake kufunga hadi kufa kwa imani kuwa baada ya kufa watakwenda mbinguni.

Polisi katika Kaunti ya Malindi yalipogunduliwa makaburi hayo wamesema, bado makaburi mengine hayajafukuliwa katika eneo linalomilikiwa na mchungaji huyo, huku tukio hilo pia likihusishwa na imani za kishirikina.

Taarifa zaidi kutoka nchini Kenya zinaeleza kuwa waumini wengine wa kanisa hilo walifariki dunia baada ya kugundulika msituni wakiwa wana njaa kali.

Mchungaji Makenzi anadaiwa kuwahi kukamatwa mara mbili, ambapo kwa mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2019 na mara ya pili mwezi Machi mwaka huu akihusishwa na vifo vya watoto.