Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeeleza kuwa kupungua kwa mfumuko huo wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2023 kumechangiwa na kupungua kwa mfumuko wa bei kwa bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwaka ulioishia mwezi Februari mwaka 2023.