Uwanja wa 974 (Stadium 974), ni miongoni mwa viwanja nane vitakavuotumika katika fainali za kombe la FIFA la Dunia mwaka huu.
Uwanja huu upo katika mji mkuu wa Qatar, Doha.
Uwanja huu umejengwa kutokana na Makontena 974, ambapo pia 974 ni code ya nchi hiyo ya Mashariki ya kati.
Sifa kubwa ya uwanja huo ni kuwa unahamishika na kwamba utahama baada ya fainali hizo za kombe la Dunia.