Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imemteua Suzan Peter Kunambi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT).
Kamati hiyo imeketi chini ya Makamu Mwenyekiti wake ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, leo Jumapili, Mei 19, 2024 katika kikao chake maalumu, kilichofanyika Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui, Zanzibar na kufanya uteuzi kwa niaba ya halmashauri Kuu ya chama hicho.