Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, – Job Ndugai, leo amemuapisha Felix Kavejuru wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mbunge wa jimbo la Buhigwe na Dkt. Florence Samizi naye kutoka CCM kuwa mbunge wa jimbo la Muhambwe, yote ya mkoani Kigoma.
Wabunge hao wameapishwa Bungeni jijini Dodoma baada ya kupata ushindi katika uchaguzi mdogo wa Ubunge uliofanyika katika majimbo hayo tarehe 16 mwezi huu.
Uchaguzi katika jimbo la Buhigwe ulifanyika baada ya aliyekuwa mbunge Dkt. Philip Mpango kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
KAVENJURU AKILA KIAPO KUWA MBUNGE WA BUHIGWE, KIGOMA pic.twitter.com/sHooefHm51
— TBCOnline (@TBConlineTZ) May 24, 2021
Katika jimbo la Muhambwe umefanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia CCM, – Atashasta Nditiye.
DKT. SAMIZI AKILA KIAPO KUWA MBUNGE WA JIMBO LA MUHAMBWE, KIGOMA pic.twitter.com/CuzdcSRHP7
— TBCOnline (@TBConlineTZ) May 24, 2021