JERRY SILAA AMWAGA CHOZI BUNGENI

0
168

Mbunge wa jimbo la Ukonga mkoani Dar es Salaam, Jerry Silaa akilia baada ya kumaliza kuchangia mjadala wa bajeti ya wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 bungeni jijini Dodoma hii leo.

Miongoni mwa sababu zilizomfanya Mbunge huyo kumwaga chozi ni kutotekelezwa kwa ahadi mbalimbali zilizotolewa kwa wananchi wakati wa uchaguzi uliopita, jambo ambalo amedai litawaweka katika mazingira magumu ya kurudi kuomba kura kwenye uchaguzi wa mwaka 2025.