Dkt. Samia mgeni rasmi siku ya Wanawake BAWACHA

0
184

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Freeman Mbowe ametangaza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake wa CHADEMA kitaifa yaliyoandaliwa na Baraza la Wanawake la chama hicho ( BAWACHA ) yatakayofanyika tarehe 8 mwezi huu mkoani Kilimanjaro.

Mbowe ametoa tangazo hilo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari jijini Arusha.

Amesema yeye ataongoza mapokezi ya Rais Samia Suluhu Hassan mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, ambapo Rais atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ambayo pia itakuwa ni Siku ya Wanawake Duniani.

Mbowe ameongeza kuwa akiwa jijini Arusha leo, amekutana na kufanya mazunguzo na Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu ndogo, Arusha ambapo wamejadili mambo mbalimbali yanayohusu demokrasia na kuendeleza maridhiano.