Dkt Mahera: Viti Malum Chadema ni halali

0
311


Akizungumza Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa uchaguzi wa tume ya taifa ya uchaguzi NEC, Dkt. Wilson Mahera Charles amesema Katibu Mkuu wa CHADEMA aliiandikia barua Tume ya taifa ya Uchaguzi tarehe 19 Novemba akiwasilisha majina kulingana na utaratibu wa kisheria.


Dokta WILSON MAHERA CHARLES amesema wabunge hao ni
halali kwani uteuzi wao umepitia katika taratibu za kisheria

Tume ya Taifa ya Uchaguzi – NEC imesema uteuzi wa wabunge 19
wa viti maalum wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo –
CHADEMA, umefuata taratibu zote za kisheria.