Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kumteua Rais Dkt. John Magufuli kugombea Urais wa Tanzania na Mama Samia Suluhu kugombea nafasi ya Makamu wa Rais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
NEC imetoa taarifa hiyo muda mfupi baada ya wagombea hao kurejesha fomu katika ofisi za taasisi hiyo zilizopo Ndejengwa jijini Dodoma.
Akizungumza mara baada ya kupokea fomu hizo, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu, Semistocles Kaijage amesema kuwa wagombea hao wamekidhi vigezo vya kisheria, na amewatakia heri katika mchakato mzima wa uchaguzi.