Chama na Miquissone waitema Simba

0
230

Klabu ya Simba Sports Club imekubaliana na maombi ya uhamisho ya wachezaji wake wawili nguli kwenda kuchezea vilabu vya nje ya Tanzania.

Kulingana na taarifa iliyotolea na Simba SC, fursa walizopata Clatous Chama na Luís Miquissone zinatokana na “mafanikio ya klabu katika Ligi ya Mabingwa Afrika” ambayo ni juhudi ya timu nzima.

Klabu imefikia uamuzi hup kwa kuzingatia maslahi mapana ya klabu hiyo na wachezaji hao na kuwapongeza kwa mchango wao katika Klabu na kuwatakia mafanikio katika hatua hii mpya kwao.

Taarifa za vituo vipya kwa wachezaji hao bado hazijawekwa wazi.