Timu ya Barcelona imeangukia pua leo katika mchezo wa ligi baada ya kubamizwa mabao 2 kwa bila dhidi ya Valencia
Barcelona imepoteza mchezo huo huku hasimu wake wa karibu Real Madrid akijiwinda kukalia usukani wa ligi hiyo
Real Madrid watakipiga dhidi ya Real Valladolid hapo kesho wakiwa na malengo yakumzidi Barcelona alama tatu kama wakishinda mchezo huo
Hadi sasa Barcelona imecheza michezo 21 na alama 43 wakati Real Madrid imecheza michezo 20 ikiwa na alama 43