Baraza la Mawaziri mwisho kufanya kazi leo

0
307

Baraza la mawaziri litakoma leo kuendelea na shughuli za kikazi mara Rais Mteule, Dk. John Magufuli atakapoapishwa katika sherehe inakayofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya kuapishwa kwa Rais Mteule, Dkt. Magufuli.

Dkt. Abbasi amesema kuwa kisheria ni kwamba Baraza la Mawazili la 2015-2020 mwisho wake ni mara tu Rais Mteule atakapoapishwa kushika kipindi chake cha pili cha miaka mitano. Majukumu yote yatafanywa na makatibu wakuu wa wizara hadi atakapotangaza baraza jipya.