Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Theopista Mallya ametoa wito kwa wananchi wa mkoa huo kutojichukulia sheria mkononi kwa kufanya vitendo vya kikatil ambavyo ni kinyume cha sheria hasa mauaji.
Kamanda Mallya ametoa wito huo wakati akitoa salamu za sikukuu ya Pasaka katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ( KKKT) Dayosisi ya Dodoma, Jimbo la Makao Makuu Usharika wa Arusha Road.
“Mwenye mamlaka ya kukatisha uhai wa mtu ni Mungu peke yake, hivyo kupitia maungamo na sala mlizofanya katika kipindi cha Mfungo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma hatutegemei kuwepo kwa matukio ya mauaji pamoja na uhalifu mwingine,” amesema Kamanda Mallya.