Zungu aiomba nyasi bandia uwanja wa shule ya Sekondari Benjamin

0
1568

Naibu Spika Azan Zungu ambaye ni mbunge wa Jimbo la ilala ameiomba Serikali kuweka nyasi za bandia kwenye uwanja wa mpira wa shule ya Sekondari Benjamin Mkapa ili kuwezesha wanafunzi wa shule hiyo kutumia kipindi chote cha mwaka.

Zungu amesema hayo kwenye Ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan shuleni hapo na kueleza kuwa uwanja umekuwa ukitumika kwa muda mchache kutokana na kutumia majani ya kupanda ambapo wanalazimika kufunga uwanja huo kupisha majani kuota tena baada kutumika kwa muda kitu kinachopelekea watumiaji kukosa fursa ya kutumia uwanja huo

Akitoa salamu za Jimbo la Ilala, Zungu amesema wilaya ya Ilala kwa asilimia 75 hadi 80 inabeba uchumi wa Taifa kutokana na ukusanyaji wa mapato lakini bado miundombinu yake ni duni na inahitaji kuboreshwa ili kuongeza tija ya upatikanaji wa mapato na kukuza uchumi wa nchi.