TFF imeitoza Yanga SC jumla ya shilingi milioni 3.85 kutokana na makosa mbalimbali yaliyotendekea katika mchezo wa Julai 3, 2021 dhidi ya Simba SC.
Katika fedha hizo Yanga imetozwa shilingi milioni tatu kwa makosa ya;
- Kutumia mageti ya Uwanja wa Uhuru kuingia Uwanja wa Benjamin Mkapa badala ya mlango maalum unaotumika na timu.
- Kutumia mlango wa chumba cha waandishi wa habari (media center) badala ya mlango maalumu unaotumiwa na timu.
- Kuingia uwanjani kupasha misuli (warm up) kwa kutumia mlango wa (gate B) ambao haukupangwa kutumika kwa namna yeyote.
- Kutumia chumba cha wafanya usafi wa uwanja kwa ajili ya kubadilisha nguo badala ya chumba maalumu cha kubadilishia nguo (dressing room)
Pia timu Yanga imetakiwa kulipa shilingi 850,000 ikiwa ni gharama ya ukarabati wa mageti yaliyovunjwa wakati wakiingia uwanjani, pamoja na makufuli ya uwanja wa Benjamin Mkapa yaliyoharibiwa katika tukio hilo.