Timu soka ya Yanga ya Jijini Dar es salaam, imefanikiwa kuingia nusu fainali kwenye mashindano ya kombe la Mapinduzi baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 na mafaande wa KMKM.
Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Amaan Zanzibar, umeshuhudia Yanga wakienda mapumziko wakiwa mbele kwa bao moja kwa nunge huku bao la Yanga likifungwa katika dakika ya 45 na Eritie Makambo.
Dakika 54 Kipindi cha pili KMKM, wakasawazisha bao hilo kupitia Abrahaman Othman Ally, kabla Feisal Salum kuiandikia Yanga bao la pili dakika ya 86.
Dakika za majeruhi Abdulharim Hamad Abdallah akifunga goli la kusawazisha kwa KMKM
Kutokana na matokeo hayo Yanga imekuwa kinara wa kundi B na itacheza hatua ya nusu fainali na mshindi wa kwanza wa kundi A