Yanga yaingia mgogoro kisa jezi mpya

0
334
Jezi Mpya za Yanga SC mashindano ya Kombe la Shirikisho la CAF

Kampuni ya SportPesa imeeleza kusikitishwa na uamuzi uliochukuliwa na Yanga SC uliokiuka makubaliano yao ya kimkataba kwa kuzindua jezi mpya zenye jina na mdhamini mwingine.

“SportPesa inapenda kuwafahamisha wateja wake na umma kuwa bado ni mdhamini Mkuu wa klabu na ina haki ya kipekee ya kuwa kifuani mwa Yanga SC kwa miaka ya soka 2022-2025,” imeeleza taarifa ya kampuni hiyo

Aidha, imeeleza kuwa Yanga ilikataa pendekezo la kutumia kauli mbiu ya kuitangaza nchi ya ‘Visit Tanzania’ kwa sababu ilikuwa tayari imeamua kuuza haki hizo bila kujali masharti ya kimkataba kati yake na SportPesa.

Kutokana na mkanganyiko huo SportPesa imesema “inahifadhi haki yake ya kuomba fidia na msaada kutoka kwa mamlaka husika kwa uharibifu uliosababishwa.

Januari 30 mwaka huu Yanga ilizindua jezi zenye mdhamini mpya ambazo zitatumika katika mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo yapo katika hatua ya makundi.