Yanga yaanza rasmi mazoezi

0
241

Wachezaji wa kikosi cha Mabingwa wa soka wa Tanzania Yanga SC kimeanza mazoezi ya kujiwinda na msimu ujao wa ligi kuu inayoatarajiwa kuanza Agosti 13 mwaka huu.

Baadhi ya wachezaji wanaounda kikosi hicho wameanza mazoezi chini ya Kocha Mkuu Mohamed Nabi katika kambi ya timu hiyo iliyopo Avic Tower Kigamboni, Mkoani Dar es salaam.

Baadhi ya wachezaji wa kigeni waliosajiliwa na klabu hiyo wameungana na wale wa zamani katika mazoezi hayo ya jana jiioni ambapo nyota wa Burkina Faso Stephanie Aziz Ki naye ameanza rasmi kazi klabuni hapo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Yanga, awali kambi ya timu yao ilikuwa ifanyike nchini Uturuki lakini wakaamua kuahirisha na kuifanya hapa nchini.