Yanga na ZANACO kukutana dimba la Mkapa

0
3417

Timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam maarufu timu ya Wananchi, tarehe 29 mwezi huu itaialika timu ya ZANACO FC kutoka Zambia katika mchezo wa kirafiki kwenye dimba la Mkapa mkoani Dar es Salaam.

Siku hiyo itakuwa ndio kilele cha wiki ya Wananchi, ambapo timu hiyo ya Yanga huitumia kufanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutambulisha wachezaji wake wapya na benchi la ufundi.