Yanga na Azam, nani kuondoka na alama tatu?

0
1399

Ni Dar es Salaam Derby leo Jumamosi katika NBC Premier League ambapo Wananchi, Yanga Afrika watakuwa Uwanja wa Azam Complex kama wenyeji wakiwakaribisha Azam FC.

Yanga SC wanaingia katika mchezo huu wakiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi, huku Azam FC ikiwa nafasi ya nne.

Wananchi wanataka alama tatu ili kuzidi kujikita kileleni, huku Azam FC nao wakizitaka hizo alama tatu ili kusogea nafasi ya tatu.

Je, ni Wananchi ama matajiri wa Chamazi, watakaoondoka na alama tatu?

Mechi hii itachezwa kuanzia saa 12:00 jioni na itatangazwa mbashara kupitia #TBCTaifa na mitandao ya kijamii ya TBC Online.