Yanga mmeipa furaha nchi

0
367

Rais Samia Suluhu Hassan ameipongeza klabu ya Yanga kwa kufanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika ukurasa wake wa Instagrama Rais Samia ameandika
”Naipongeza Klabu ya Yanga kwa kufanya vyema katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), na kufanikiwa kufuzu hatua ya Robo Fainali.”

Na kuongeza kuwa
“Mafanikio haya yameandika historia kubwa kwa klabu na sekta ya michezo. Mmeleta furaha kwa mamilioni ya mashabiki wenu na Watanzania kwa ujumla.”

Kufuatia ushindi huo wa Yanga wa mabao 4 dhidi ya CR Belouzdad ya Algeria, Rais Samia Suluhu Hassan Jumamosi. Februari 24, 2024 kupitia wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo alikabidhi shilingi Milioni 20 kwa klabu hiyo kama ilivyo ada kwa utaratibu wa Goli la Mama.