Waziri Mkuu: Timu za Taifa ziendelee kupambana

0
232

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ametoa wito kwa timu nyingine za Taifa kuendelea kufanya vizuri katika michuano mbalimbali kwani serikali imekuwa ikisimamia maendeleo ya timu hizo ili kufanya vizuri katika anga za kimataifa

Wito huo umetolewa leo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa halfa ya kuipongeza Timu ya Taifa ya mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu Tembo Warriors na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa motisha ya shillingi milioni 150 kwa wachezaji waliofanikiwa kusonga mbele timu hiyo kufuzu katika michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika mwakani nchini Uturuki