Kocha wa timu ya Coastal Union ya Tanga, Juma Mgunda anaamini wachezaji wake wanafanya mazoezi binafsi na kufuata maagizo yote aliyowapatia wakati huu ambapo ligi imesimama kutokana na janga la Corona.
Akiongea na TBC, Jijini Tanga, Mgunda amesema wakati huu wachezaji hao inabidi wafanye mazoezi mepesi ambayo yatalinda viwango vyao
Ligi kuu soka Tanzania bara pamoja na shughuli zote za kimichezo zimesimama kwa muda ili kuepsha hatari ya maambukizi ya virusi vya COVID 19 vinavyosababisha ugonjwa wa Corona.