Viwanja vitano vyapigwa stop ligi kuu

0
322

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limezuia kutumika kwa viwanja vitano kwenye mechi za ligi kuu Tanzania Bara.

TFF imefikia uamuzi huo kutokana na viwanja hivyo kutokidhi vigezo, huku vingine vitatu vitaruhusiwa baada ya marekebisho yanayoendelea kukamilika na kupitishwa na kamati ya leseni za klabu.

Katika taarifa yake TFF imevitaja viwanja vilivyozuiwa kutumika kuwa ni Mkwakwani -Tanga, Nyankumbu Girls – Geita, Ushirika – Moshi, Mabatini – Pwani na Jamhuri – Dodoma.

Viwanja ambavyo viko kwenye marekebisho ni Majaliwa – Lindi, Sokoine – Mbeya na Kaitaba – Kagera.

Taarifa hiyo ya TFF pia imevitaja viwanja vilivyopitishwa kutumika kwenye ligi kuu Tanzania Bara kuwa ni Benjamin Mkapa – Dar es Salaam, Kirumba – Mwanza, Chamazi – Dar es Salaam, Highland Estate – Mbeya, Karatu – Arusha, Liti – Singida, Manungu – Morogoro, Amri Abeid – Arusha na Uhuru -Dar es Salaam.