Viwango vya ubora vya FIFA kwa timu za wanaume

0
2344

Michuani ya AFCON iliyomalizika mapema mwezi huu imekuwa na mchango mkubwa kwa baadhi ya timu kupanda katika viwango vya FIFA kutokana na ubora wa timu hizo kwenye mashindano hayo.

Nigeria ambayo ilifika hatua ya fainali ya AFCON imepanda kwa alama 14, huku mabingwa, Ivory Coast wakipanda kwa alama 10.

Wakati wao wakisherehekea kupanda baadhi ya timu zilipoteza alama zikiwemo Tunisia na Algeria ambazo zimeshuka kwa alama 13 kila moja.

Aidha, kwa upande wa Tanzania, imepanda kwa nafasi mbili kutoka nafasi ya 121 iliyokuwepo Desemba 2023 hadi nafasi ya 119 Februari 2024.