Vipers kuwakosa nyota wake dhidi ya Simba

0
181

Msafara wa wachezaji 20 wa Vipers SC umewasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba SC.

Katika mchezo huo utakaochezwa Machi 7 mwaka huu saa 1:00 jioni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Vipers itawakosa nyota wake akiwemo Murushid Juuko, Milton Karisa na Bright Anukani.

Juuko ana majeraha ya kifundo cha mguu, nahodha Karisa ana majeraha ya msuli wa paja na Anukani anaumwa malaria, taarifa ya klabu imeeleza.

Mchezo huo ambao utakuwa ni vita ya faru wawili waliojeruhiwa mwituni utakuwa wakusisimua kwani kila timu inasaka alama tatu kuweka hai zaidi matumaini yao ya kufuzu hatua ya robo fainali ya mashindano hayo.

Katika mchezo wa kwanza nchini Uganda, Simba iliondoka na alama 3 kwa ushindi wa goli 1-0, goli la Henock Inonga dakika ya 20