Uwanja wa Mtibwa Sugar wafungiwa

0
308

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeufungia uwanja wa Manungu Complex uliopo Turiani mkoani Morogoro kutumika kwa michezo ya ligi.

Uwanja huo unaomilikiwa na klabu ya Mtibwa Sugar umefungiwa hadi hapo utakapofanyiwa marekebisho kwenye eneo la kuchezea, kisha ukaguliwe ili kuendelea kutumika kwa michezo ya ligi.

Kwa uamuzi huo, Mtibwa Sugar imetakiwa kuchagua uwanja mwingine kwa ajili ya michezo ya nyumbani ya ligi.

Wakati ligi ikianza Mtibwa haikuwa ikitumia uwanja huo, baada ya maboresho imeutumia kwa michezo miwili na kuonekana kutokidhi vigezo.