Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Abdallah Ulega ameshiriki mbio za mwendo wa pole ( jogging) pamoja na mazoezi ya viungo wakati wa fainali ya mashindano ya Kombe la Nyumba ni Choo kwa Wilaya ya Kigoma Mjini yaliyofanyika leo katika uwanja wa Mwanga mjini Kigoma.
Wakati wa fainali hizo, Naibu Waziri Ulega aliwapongeza viongozi wa Mkoa na Wilaya ya Kigoma kwa juhudi kubwa za kuibua na kukuza vipaji vya michezo na sanaa.
” Kigoma ni kitovu cha vipaji vya michezo na sanaa hapa nchini ni matumaini yangu msimu ujao Kigoma itakuwa na timu ya mpira wa miguu kwenye ligi kuu”
“Nimefuatilia mchezo wa fainali kwa umakini na nimeona vipaji vingi vya hali ya juu kabisa, vijana wanajituma na wanacheza mpira wa kuvutia”, amesema Ulega
Naibu Waziri Ulega pia amegawa zawadi kwa washindi mbalimbali wa mashindano hayo yanayo ratibiwa na Wizara ya Afya, Ustawahi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na TFF.