Turkaslan afariki katika tetemeko Uturuki

0
317

Mlinda mlango raia wa Uturuki, Ahmet Eyup Turkaslan amefariki dunia kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea Jumatatu nchini kwao, klabu yake ya Yeni Malatyaspor imethibitisha.

Turkaslan ni miongoni mwa watu takribani 9,000 ambao wamefariki dunia hadi sasa nchini Uturuki na Syria kufuatia tetemeko la ardhi.

“Kipa wetu alifariki baada ya tetemeko la ardhi. Pumzika kwa amani, hatutakusahau,” klabu hiyo imeandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Turkaslan, 28, ameichezea klabu hiyo inayoshiriki ligi daraja la pili michezo sita tangu alipojiunga nayo mwaka 2021.

Wachezaji mbalimbali wametoa rambirambi kufuatia kifo cha mwanasoka huyo.