Timu ya Taifa ya Burundi itatumia Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wake wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeeleza kuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Burundi (FBB) liliwasiliaha ombi kwa kutaka kutumia uwanja huo, na wamekubali baada ya kushauriana na serikali.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Machi 26 mwaka huu.