TFF yatupilia mbali tena ombi la Fei Toto

0
483

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imetupilia mbali maombi ya Fei Toto ya kuvunja mkataba wake na Yanga SC.

Kamati hiyo iliyokutana Mei 4 mwaka huu imesema kuwa tayari ilishaamua juu ya uhalali wa mkataba wa mchezaji huyo na klabu yake kwamba ana mkataba unaoendelea hadi mwaka 2024.

Taarifa ya kamati imeeleza zaidi kuwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za uvunjani wa mkataba, mchezaji lazima aanze na majadiliano na klabu yake ambayo ndio mwenye haki naye.