Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imetupilia mbali shauri la mapitio ya uamuzi wake wa Januari 9, 2023 kati ya Feisal Salum dhid ya Yanga SC.
Taarifa hiyo ya kamati ambayo imetokana na kikao cha leo cha shauri hilo imeeleza kuwa shauri hilo halina msingi wa kisheria kushawishi kamati kubadili maamuzi yake yaliyotolewa awali.
Katika uamuzi wake wa awali TFF ilieleza kuwa bado Feisal Salum ‘Fei Toto’ ni mchezaji halali wa klabu hiyo kwa mujibu wa mkataba uliopo na waajiri wake.
Klabu ya Yanga iliwasilisha malalamiko yake mbele ya kamati hiyo kupinga hatua za mchezaji huyo kuvunja mkataba kati yao bila ya kuwashirikisha.