TFF yaaswa kuulinda mpira wa miguu

0
208

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Mohamed AbdulAziz amelitaka shirikisho hilo kuulinda mpira wa miguu kutokana na mchango wake mkubwa katika uchumi.

AbdulAziz ametoa wito huo wakati wa kufungua mkutano mkuu wa 17 wa kawaida wa Shirikisho la Soka Tanzania unaofanyika jijini Mwanza.

Amesema kuwa kwa sasa mpira wa miguu umekuwa na msisimko mkubwa na kuwavutia watu wengi, hivyo ni jukumu la TFF kulinda na kupokea changamoto zote ili kuboresha usimamizi wake.

AbdulAziz ameongeza kuwa mafanikio yanayoonekana katika mpira wa miguu ni matokeo ya usimamizi mzuri wa TFF, hivyo wanapaswa kuusimamia na kuuendeleza kwa manufaa ya Taifa.