Timu ya Taifa ya soka ya Argentina imeshindwa kutamba leo mbele ya timu ya Taifa ya Saudi Arabia katika michuano ya Kombe la FIFA la nchini Qatar, baada ya teknolojia ya usaidizi wa maamuzi ya mchezo uwanjani (VAR) kukataa bao la Argentina wakati wakicheza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Saudi Arabia.
Hadi dakika tisini za mtanange huo Saudi Arabia wameibuka na ushindi wa mabao 2 kwa 1 baada ya kutoka nyuma kwa bao moja na kuongeza bao la pili katika kipindi cha pili cha mchezo huo uliopigwa katika dimba la Lusail.
Ushindi huo unaipa timu ya Taifa ya Saudi Arabia alama 3 muhimu na kukaa kileleni mwa msimamo wa kundi C huku timu ya Taifa ya Argentina ikiachwa mkiani bila alama yoyote katika mchezo wa kundi C kwenye michuano hiyo ya Kombe la FIFA la Dunia nchini Qatar